Jumatano 8 Julai 2026 - 12:40
Hafla Rasmi ya Kuusindikiza Mwili wa Imam Shahidi Khamenei Yaanza Najaf Ashraf kwa Ushiriki wa Viongozi Wakuu

Hawza/ Hafla rasmi ya mazishi ya mwili wa Imam Shahidi Sayyid Ali Khamenei imeanza katika mji wa Najaf Ashraf, kwa kuhudhuriwa na viongozi wa ngazi za juu wa nchi mbili.

Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, hafla rasmi ya mazishi ya mwili wa Imam Shahidi Sayyid Ali Khamenei, aliyekuwa Kiongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, imeanza katika mji wa Najaf Ashraf kwa ushiriki wa viongozi wa ngazi za juu kutoka nchi mbili.

Ofisi ya Waziri Mkuu wa Iraq imetangaza kuwa hafla rasmi ya mapokezi ya mwili wake ilifanyika kwa uwepo wa Ali Falih al-Zaidi, Waziri Mkuu wa Iraq, na Masoud Pezeshkian, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, pamoja na ujumbe wao ulioandamana nao. Hafla hiyo pia ilishuhudiwa na ushiriki mkubwa wa viongozi wa kisiasa, kidini, viongozi wa makabila na wananchi wa Iraq katika mji wa Najaf Ashraf.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha